1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Uchaguzi Tunisia: Rais Saied atarajia muhula wa pili

6 Oktoba 2024

Raia wa Tunisia wanafanya uchaguzi wa rais Jumapili bila upinzani wa kweli dhidi ya rais aliyeko madarakani Kais Saied ambaye anatarajiwa kushinda muhula wa pili.

Tunisia | Uchaguzi wa Rais
Uchaguzi wa rais TunisiaPicha: Zoubeir Souissi/REUTERS

Vituo vya kupiga kura vilifunguliwa rasmi mwendo wa saa mbili asubuhi na vinatarajiwa kufungwa saa kumi na mbili jioni.

Bodi inayosimamia uchaguzi nchini humo (ISIE) imesema matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutangazwa kabla ya Jumatano lakini huenda yakatolewa mapema.

Kabla ya siku ya kupiga kura, hakukuwa na mikutano ya kampeni au mijadala ya hadhara, na takriban mabango yote ya kampeni katika mitaa ya jiji yalikuwa ya Saied.

Shirika la Human Rights Watch limesema zaidi ya watu 170 wanashikiliwa na vyombo vya usalama nchini Tunisia kwa misingi ya kisiasa au kwa kutekeleza haki zao za kimsingi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW