Uchaguzi wa rais mpya wafanyika Nagorno Karabakh
9 Septemba 2023Azerbaijan imeutaja uchaguzi huo kuwa hatua nyingine ya uchokozi mkubwa na ukiukaji wa wazi wa uhuru wake na uadilifu wa eneo hilo. Mkuu wa baraza la usalama la serikali hiyo ya uasi Samvel Shahramanyan, anaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kumrithi Arayik Harutyunyan aliyejiuzulu mnamo Septemba mosi.
Armenia na Azerbaijan zimekuwa zikishtumiana kwa mashambulizi ya kuvuka mpaka
Katika miezi ya hivi karibuni, Armenia na Azerbaijan zimekuwa zikishtumiana kwa mashambulizi ya kuvuka mpaka.Armenia imeonya kuhusu hatari ya mzozo mpya, ikisema Azerbaijan imekuwa ikikusanya wanajeshi kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hizo na karibu na Nagorno-Karabakh. Siku ya Ijumaa, wizara ya mambo ya nje ya Azerbaijan iliishutumu Armenia kwa kukiuka makubaliano ya awali na kuanza kufanya uchokozi wa namna mbalimbali ukiwemo wa kisiasa na wa kijeshi.