Uchaguzi wa bunge Burundi wafanyika leo
23 Julai 2010Nchini Burundi,uchaguzi wa wabunge umeanza rasmi hii leo baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa mapema asubuhi. Ifahamike kuwa vyama vya upinzani vinaususia uchaguzi huu kwasababu ya malalamiko yao kuwa mipango haijakamilika. Hata hivyo chama tawala cha CNDD-FDD cha Rais Nkurunziza kimewasilisha wagombea wake na ni vyama vidogo vya upinzani vinavyoshiriki katika zoezi hilo.
Uchaguzi huu unafanyika katika mazingira ya hofu baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kutisha kuwa huenda ikaishambulia Burundi kwasababu ya mchango wake katika ujumbe wa Somalia wa kulinda amani.
Ili kupata picha kamili ya jinsi shughuli inavyokwenda Thelma Mwadzaya alizungumza na mwandishi wetu Amida Issa aliyekuwa kwenye kituo kimoja cha kupigia kura mjini Bujumbura. Anaanza kwa kulielezea zoezi lenyewe.