1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Bunge la Umoja wa Ulaya

Abdu Said Mtullya8 Juni 2009

Vyama vikuu vimethibiti kuwa imara katika bunge laUmoja wa Ulaya.

Wananchi wakivinjari kwenye njia ya kuelekea kwenye bunge la Umoja wa Ulaya mjini BrusselsPicha: AP

BERLIN:
Vyama vinavyotawala katika  serikali  ya mseto  nchini Ujerumani  vya CDU na CSU vimeongoza katika uchaguzi  wa bunge  la Umoja  wa Ulaya kwa kupata asilimia 37. 9 ya kura.

Chama kingine kilichomo katika serikali ya hiyo  cha SPD  hakikufanya vizuri katika  uchaguzi  huo na kimepata asilimia 20. 8 ya kura.

Vyama  vya  upinzani  vya  FDP,Kijani na cha  mrengo wa shoto vimefanikiwa kuongeza  idadi ya  viti .

Katika mandhari ya Ulaya  kwa jumla vyama  vya  mrengo mkali wa kulia vimepata  mafanikio  makubwa  katika uchaguzi  wa  bunge  la  Umoja wa Ulaya.


Nchini Uingereza chama  cha kibaguzi BNP kimefanikiwa  kupata  kiti  katika bunge hilo kwa  mara ya kwanza.


Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW