1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Bunge nchini Ufaransa

Mutasa Omar18 Juni 2007

Chama cha UPM (union for popular movement) cha Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa kimeshinda katika uchaguzi wa Bunge jana nchini Ufaransa.

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa
Rais Nicolas Sarkozy wa UfaransaPicha: picture alliance/dpa

Hata hivo chama hicho licha ya kunyakua viti vingi bungeni kimempoteza moja ya mgombea wake muhimu kwenye uchaguzi huo na imebidi sasa ajiuzulu wadhifa wake wa uwaziri.

Chama cha Rais Nicolas Sarkozy UMP kilijinyakulia viti 314 kati ya viti 577. Katika uchaguzi uliopita chama cha UMP kilikua na wabunge 359 hivo safari hii kimepoteza viti 45, lakini bado kitakua na uwezo wa kutoa maamuzi ya mojo kwa moja bungeni.

Chama cha kisoshalisti kinacho ongozwa na Francois Hollande kilijiongezea viti zaidi kutoka viti 149 hadi viti 185 huku chama

cha New Center, kinachoshirikiana na chama cha UMP cha Rais Sarkozy kikajipatia viti 22.

Francois Bayrou wa chama cha Democratic Party aliweza kujishindia kiti kimoja kati ya viti vitatu walivyojipatia, huku mshirika mkuu wa Rais Nicolas Sarkozy, Alain Juppe mwenye umri wa miaka 61 ambae ni waziri wa Mazingira, akishindwa na msoshalisti katika bunge la Bordeaux, na leo Alain Juppe amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Nicolas Sarkozy kufatia uamuzi uliotolewa, kua waziri yoyote atakae shindwa kwenye uchaguzi huu itabidi ajiuzuulu.

Moja ya sababu ambazo huenda zimepelekea Alain Juppe ashindwe kwenye uchaguzi huu,ni kwamba amekua na kashfa ya ubadhirifu wa fedha katika chama tawala cha UMP.

Waziri mkuu Francois Fio amewasilisha waraka wa kujiuzulu kwake na serekali yake kwa Rais Nicolas Sarkozy aliemtaka aunde serekali mpya .

Gazeti la mrengo wa kihafidhina, Le Figaro limeuita uchaguzi huu kama wa kukubalika mbele ya wafaransa, lakini wengi ya wapiga kura wakifaransa, wamekua wakilalamika kua huenda Serekali ya Ufaransa ikaongeza kodi ziada ya bidhaa VAT.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW