1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UCHAGUZI WA BUNGE RUSSIA:

7 Desemba 2003
MOSCOW: Uchaguzi wa bunge-Duma umeanza nchini Russia chini ya ulinzi mkali baada ya treni ya abiria kushambuliwa na bomu siku ya Ijumaa karibu na jamhuri ya Chechnya.Kiasi ya watu milioni 110 wana haki ya kupiga kura kuwachagua wajumbe kutoka vyama 18 wanaopigania viti 450 vya Duma.Wachunguzi wa maoni ya wapiga kura wanasema chama cha Rais Vladimr Putin "United Russia" huenda kikapata kura zaidi kuhusika na suala la sheria na amani.Upigaji kura utamalizika leo jioni na matokeo ya mwanzo yanatarajiwa mapema kesho asubuhi.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW