Uchaguzi wa Bunge Urusi
7 Desemba 2003Matangazo
MOSKO: Uchaguzi wa bunge unaendelea Urusi chini ya hatua kali za usalama. Kura hiyo inatazamwa pia kama mtihani kwa uchaguzi ujao wa Rais hapo mwezi wa Machi mwakani. Kwa kufuatana na matokeo ya kura ya maoni, chama kinachojiita "Mwungano wa Urusi", kinachoungwa mkono na rais Vladimir Putin kinatazamiwa kushinda uchaguzi. Pia ziko ishara kuwa nafasi ya pili itachukuliwa na Chama cha Kikomunisti. Upande wa pili, vyama vidogo vidogo vya kiliberali havina uhakika iwapo vitaweza kuuvuka ule mpaka wa asili miya 5 ya kura zinayohitajiwa kuingia bungeni. Maafisa wa uchaguzi wameripoti kuwa hadi sasa kura inaendelea kwa usalama. Warusi wapatao miliyoni 110 wana haki ya kupiga kura na kuchagua baina ya vyama 18 vinavyogombea jumla ya viti 450 bungeni.
