Uchaguzi wa DRC huenda usifanyike Jumapili
20 Desemba 2018Tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo imesema uchaguzi uliopangwa kufanyika siku ya Jumapili hautafanyika na inatoa wito wa kuahirishwa.
Afisa kutoka upinzani Jacquemin Shabani ameliambia shirika la habari la Ujerumani dpa kuwa uchaguzi hautafanyika, na kwamba hivyo ndio rais wa tume ya uchaguzi alivyowaambia.
Anaomba uchaguzi huo uahirishwe, amesema Shabani, afisa kutoka chama cha mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi huo Felix Tshisekedi. Uchaguzi huo tayari ulicheleweshwa kwa miaka miwili na rais Joseph Kabila, ambaye yuko madarakani kwa miaka 17 sasa.
Mgombea wa chama tawala cha rais kabila Emmanuel Ramazani Shadary anapambana na wagombea wawili wa upinzani , Tshisekedi na martin Fayulu.