Uchaguzi wa Hong Kong hatihati kuahirishwa
31 Julai 2020Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam anatarajiwa hii leo kutangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa bunge la mji huo wa Septemba 6, kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Uamuzi huo utakuwa pigo kwa upande wa upinzani unaopigania demokrasia Hong Kong, ambao ulikuwa na mataumaini ya kushinda wingi wa viti bungeni.
Unafanyika katika kipindi cha shera mpya na kali ya usalama
Uchaguzi huo utakuwa wa kwanza tangu China ilipotangaza sheria mpya ya usalama wa kitaifa, ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha jela. China imesema sheria hiyo itatumika dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchochezi, njama za kujitenga, ugaidi na uingiliaji kati wa mataifa ya kigeni.
Soma zaidi: China yasitisha ushirikiano wa kisheria kati ya HK na nchi kadhaa
Serikali Kuu ya China na ya Hong Kong zimesema sheria hiyo haitotumika kukandamiza uhuru wa raia wa Hong Kong, bali inahitajika kurejesha utulivu baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya vurugu ya mwaka jana ya kuipinga serikali.