1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa jimbo la Hessen

Scheschkewitz, Daniel25 Januari 2008

Waziri mkuu wa jimbo la Hessen ROland Koch an akabiliwa na kishindo kutoka vyama vya mrengo wa shoto

Deutschland Hessen Landtagswahlen Landtag in Wiesbaden
Bunge la Hessen mjini WiesbadenPicha: AP



Wapiga kura wa jimbo la Hessen wanateremka vituoni kesho kulichagua bunge lao.Waziri mkuu anaemaliza wadhifa wake Roland Koch wa kutoka chama cha Christian Democratic anaonyesha anabanwa.Anakabiliwa na mtihani mkubwa kutoka mrengo wa shoto  baada ya kulizusha suala la "uhalifu miongoni mwa vijana wenye asili ya kigeni.


Jimbo la Hessen,mojawapo ya majimbo 16 ya Ujerumani linajikuta kati kati ya shirikisho la jamhuri ya Ujerumani.Likiwa na wakaazi zaidi ya milioni sita,Hessen ni jimbo la nne kwa ukubwa,nyuma ya jimbo la mto Rhine North Rhine Westfalia,Bayern,Baden-Württemberg na Niedersachsen.

Jimbo la Hessen ni muhimu kiuchumi na katika jiji la Frankfurt, ndiko yanakokutikana makao makuu ya benki za Ujeruman na benki kuu ya Ulaya na kitovu cha Ulaya kutokana na kiwanja chake cha ndege cha kimataifa-cha pili kwa ukubwa barani Ulaya baada ya kile cha Heathrow cha mjini London.

Frankfurt  pia ni jiji la mchanganyiko wa tamaduni tofauti.


Uchaguzi wa kesho katika jimbo la Hesse unapewa umuhimu mkubwa kupindukia hata kijimbo,kwasababu kampeni ya uchaguzi ya waziri mkuu Roland Koch wa chama cha Christian Democratic-CDU,anaelitawala jimbo hilo tangu mwaka 1999,ililenga zaidi suala la uhalifu miongoni mwa vijana wenye asili ya kigeni.Zaidi ya hayo,pindi  chama cha Die Linke kikifanikiwa kukiuka kiunzi cha asili mia tano na kuingia katika bunge la mjini Wiesbaden,kwa mara ya kwanza jimbo la "tambarare" litajikuta likitawaliwa na serikali ya mrengo wa shoto itakayowaleta pamoja wana Social Democratic wa SPD,walinzi wa mazingira Die Grüne na Die Linke.


Chama cha CDU ndicho pekee  kilichokua kikitawala mjini Wiesbaden.Katika kampeni za uchaguzi mwaka huu,waziri mkuu anaemaliza wadhifa wake Roland Koch alichochea mjadala alipolizusha suala la uhalifu miongoni mwa vijana wenye asili ya kigeni humu nchini.


"Karibu nusu ya kadhia za uhalifu na matumizi ya nguvu zinafanywa na vijana wenye umri wa chini ya miaka 21.Huo ni upande wa visa vya uhalifu miongoni mwa vijana.Na kati ya visa hivyo ,nusu vinafanywa na vijana wanaotokana na wahamiaji."


Kwa kutoa hoja hizo Roland Koch alichochoea mjadala kote nchini Ujerumani na ambao hatima yake bado haijulikani.Kwa sasa  viti vya upande wa upinzani katika bunge la mjini Wiesbaden vinakaliwa na waliberali wa FDP,wasoshial Democratic wa SPD na walinzi wa mazingira Die Grüne.Wote hao walimkosoa Roland Koch kutaka  kujipatia umaarufu tuu wakisema hoja zake kuhusu uhalifu miongoni mwa vijana wenye asili ya kigeni ni za kibaguzi.Roland Koch ameshawahi kushinda uchaguzi wa jimbo la Hessen miaka minane iliyopita kutokana na hoja zake dhidi ya wageni kukubaliwa uraia wa nchi mbili.


Sera za shule nchini Ujerumani ni jukumu la serikali kuu lakini safari hii sera hiyo imepewa umuhimu katika kampeni ya uchaguzi ya chama cha Social Democratic na mgombea wake bibi Andrea Yipsilanti.Anapigania mfumo wa shule ubadilishwe nchini Ujerumani.


"Tuna tatizo hivi sasa kwa vile kuanzia darasa la nne inabidi iamuliwe mtoto atafuata mfumo wa masomo wa aina gani.Lakini nani anaweza kumpima mtoto wa miaka kumi na kuashiria kama ataweza baadae kufanya mtihani wa kidato cha sita au la?Ndio maana tunataka mfumo bora wa elimu.!"


Kwa mara ya kwanza inaaminiwa kwamba vyama vya CDU,SPD,FDP na Die Grüne vitajikuta vinaketi pamoja na chama cha tano bungeni-chama acha mrengo wa shoto Di Linke kinachopewa nafasi nzuri ya kukiuka kiunzi cha asili mia tano.









Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW