1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa jimbo la Saxony-Anhalt mtihani kwa chama cha CDU

Zainab Aziz Mhariri: Saumu Njama
6 Juni 2021

Raia milioni 1.8 katika jimbo la Saxony-Anhalt la mashariki mwa Ujerumani wanapiga kura kulichagua bunge jipya la jimbo hilo leo Jumapili. Reiner Haseloff wa CDU bado anayo nafasi kubwa ya kuendelea kuongoza,

Deutschland Landtagswahl Baden-Württemberg
Picha: Wolfgang Rattay/REUTERS

Chama cha Christian Democratic Union, CDU cha Kansela Angela Merkel kinakabiliwa na ushindani mkali wa chama cha mrengo mkali wa kulia, kinachojiita chama mbadala kwa Ujerumani, AfD.

Uchaguzi wa leo ni kipimo kwa chama cha CDU na unaweza kuwa pigo kwa mgombea wa ukansela wa chama hicho bwana Armin Laschet anayetarajia kumrithi kansela Angela Merkel.

Utafiti wa maoni unaonyesha chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD kipo asilimia moja tu nyuma ya chama cha CDU.

Waziri Mkuu wa jimbo la Saxony-Anhalt (CDU) Reiner HaseloffPicha: Getty Images/M. Schmidt

Kansela Angela Merkel, aliye madarakani tangu 2005, anaondoka baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba.

Wagombea kutoka vyama 22 wanawania kuwakilisha vyama vyao katika bunge la jimbo la Saxony-Anhalt. Kwa muda wa miaka mitano jimbo hilo la Ujerumani Mashariki, limekuwa likiongozwa na serikali ya mseto ya vyama vya Christian Democratic (CDU), chama cha Walinzi wa Mazingira (Greens) na chama cha Social Democratic (SPD)

Mchambuzi wa maswala ya kisasa kutoka chou kikuu Huria cha Berlin Hajo Funke amesema iwapo chama cha mrengo mkali wa kulia AfD kitashinda kwenye uchaguzi wa leo matokeo hayo yatakuwa pigo kubwa kwa chama cha kihafidhina cha CDU kinachongozwa na kansela Angela Merkel na kumdhoofisha mgombea ukansela wa chama hicho bwana Armin Laschet katika uchaguzi mkuu nchini Ujerumani mnamo Septemba 26.

Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: bundeskanzlerin.de

Chama cha CDU Merkel kimeongoza katika jimbo hilo la mashariki mwa Ujerumani kwa miongo kadhaa, tangu kuungana tena kwa Ujerumani mnamo mwaka 1990.

Hata hivyo chama cha mrengo mkali wa kulia AfD kiliimarika katika uchaguzi wa jimbo wa mwaka 2016, kutokana na kulitumia swala la wakimbnizi. Mnamo mwaka 2015 kansela Angela Merkel aliruhusu kuingia nchini Ujerumani wimbi la wahamiaji kutoka nchi zilizokumbwa na mizozo kama Syria.

Mchambuzi wa maswala ya kisiasa Oskar Niedermayer amesema wapiga kura wa mashariki ya Ujerumani wana muelekeo wa kihahafidhina na kizalendo zaidi kuliko wenzao wa upande wa magharibi.

Mchambuzi huyo amesema ukweli ni kwamba wengi wa wakaazi wa Saxony-Anhalt bado wanataka kuongozwa na chama cha CDU, lakini pia wapo wengi wanaiona serikali ya muungano wa vyama vinne, ambavyo nia yao ni kukinyima nafasi serikalini chama cha AfD, sio hatua ya kidemokrasia, na sio tu jimboni humo, bali kwa Ujerumani nzima.

Mgombea wa Ukansela wa chama cha CDU Armin LaschetPicha: Michael Sohn/AP Photo/picture alliance

Amesema hii inamaanisha kuwa chama cha CDU kinapaswa kuwa na vipaumbele tofauti katikam sera zake kwa mashariki na magharibi ikiwa kinataka kuidumisha ngome yake kubwa ya wafuasi wanaokiunga mkono chama hicho ambapo mchambuzi huyo Niedermayer anasema "Hiyo sio kazi rahisi."

Vyanzo:/AFP/DPA

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW