Uchaguzi wa Kongo
1 Agosti 2006
„Hukumu juu ya jinsi uchaguzi ulivyokwenda nchini J.K.Kongo barabara,lakini ni hukumu ya muda tu-sio ya mwisho.Kwa mara ya kwanza tangu kupita miaka 40,wakongomani wameweza tena kuwachagua waakilishi wao kwa njia ya kidemokrasi na hakujazuka machafuko yalaiohofiwa kuzuka.
Swali ni je, uchaguzi huu ungepita hivyo salama –usalaimini bila ya kuwapo kwa majeshi ya kigeni-miongoni mwayo yale ya Ujerumani ? Mtihani hasa juu ya uchaguzi wa Kongo unakuja na pia hata kwa majeshi ya kigeni yaliowekwa humo nchini“-laandika gazeti.
Gazeti la LANDESZEITUNG kutoka Lüneburg laonya:
Ni mapema kushangiria .Kupita uchaguzi wa Kongo kwa uhuru na amani ni mafanikio ya kazi ya vikosi vya UM na UU.Mtihani hasa kwa vikosi hivyo yawezekana uko njiani pale vikundi vitakavyoshindwa uchaguzi huu vitakapotaka kunyakua kwa nguvu madaraka.
Endapo vikosi vya UM na UU vikin’gatuka Kongo na mapema,uchaguzi wa juzi si chochote zaidi ya matumaini yaliokwenda arijojo katika moyo wa bara la Afrika-laandika LANDESZEITUNG.
Ama gazeti la LAUSITZER RUNDSCHAU kutoka mji wa Cottbus lakitupia macho kikosi cha kushambulia cha UU nchini Kongo:
Linasema gazeti kuwa kikosi hiki jukumu lake ni kuhakikisha uchaguzi huru-uchaguzi ambao unawapa wakongomani matumaini pekee ya kukomesha maafa yanayotokana na vita vya miaka mingi vya umwagaji damu nchini Kongo .
Matumaini haya yana ukubwa gani,kumeoneshwa na kushiriki kwa wingi mno na bila maonevu katika uchaguzi kwa wakongomani wenyewe.
Kutakuwepo baadae walioshindwa–yaani wale wenye majeshi ya wanamgambo.
Kuwadhibiti hawa kwa kuweka tu majeshi na ikibidi hata kupambana nao hilo ndilo jukumu la Jumuiya ya kimataifa na hata wanajeshi watu huko Afrika.Ni jukumu la hatari lakini ni lenye faida-laandika LAUSITZER RUNDSCHAU kutoka Cottbus.
Gazeti la TAGEBLATT kutoka Minden lina wasi wasi .Laandika kwamba, kuandaa uchaguzi wa kidemokrasi chini ya hali ya Kongo na kwa mafanikio bila ya shaka ni ufanisi wa juhudi za kimataifa.Matokeo hasa ya utaratibu huu yataonekana pale wale wote waliohusika n a zaidi walioshindwa na wafuasi wao wakiruhusu kuhesabiwa kura kikawaida na mwishoe kuridhia matokeo yake.
Mwishoe juu ya mada hii gazeti la NEUE WESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld laandika:
„Kunahitajika ufumbuzi mkubwa ili kukifumbua kitandawili cha Kongo na kuipatia amani ya kweli.Kwani hujuma za maadui kutoka jirani Uganda,Ruanda na Burundi,zikichochea mapigano mapya tena na tena mnamo miaka ya nyuma.Kuwabainishia wakongomani mustakbala mwema,kunawezekana tu chini ya usukani wa Umoja wa Mataifa“-lasema NEUE WESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld.