Uchaguzi wa Kosovo
12 Desemba 2010Wapiga kura nchini Kosovo leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza, tangu Kosovo kujitangazia uhuru wake kutoka Serbia mwaka 2008. Wagombea wakuu katika uchaguzi huo ni Waziri Mkuu Hashim Shah-Chi na mshirika wake wa zamani katika serikali ya mseto Isa Mustafa ambaye ni meya wa mji mkuu Pristina. Mustafa anatumia ngao ya vita dhidi ya rushwa katika kampeini yake, kwa lengo la kujipatia kura kutokana na hali mbaya ya uchumi ambayo imewavunja moyo wananchi wengi wa Kosovo. Katika uchunguzi mpya wa maoni uliotolewa unaonyesha kuwa asilia mia 73 ya raia wa Kosovo wanadhani kuwa rushwa imekuwa mbaya zaidi chini ya utawala wa Sha-Chi ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu ijitangazie uhuru wake. Tangu kujitangaza taifa huru Kosovo imetambuliwa na mataifa 72, ikiwemo Marekani na nchi 22 za Umoja wa Ulaya ispokuwa tano za Umoja huo wenye wanachama 27. Umoja wa Ulaya umeitaka Kosovo kuhakikisha kuwa uchaguzi wake huo wa kwanza unakuwa huru na wa haki.