1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa mapema Ujerumani kufanyika Februari 23 mwakani

12 Novemba 2024

Vyama vikuu vya kisiasa nchini Ujerumani vimefikia makubaliano ya tarehe ya uchaguzi wa mapema, kufuatia kuvunjika kwa muungano tawala wa Kansela Olaf Scholz.

Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz wa chama cha SPD Picha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance

Ripoti za vyombo vya habari zinasema, Ujerumani sasa itafanya uchaguzi wa mapema, mnamo Februari 23 mwakani. 

Duru zinasema makubaliano kuhusu tarehe ya uchaguzi yamefikiwa Jumanne (12.11.2024) kati ya viongozi wa bunge kutoka chama cha Scholz cha Social Democrats (SPD) na kile cha Kihafidhina cha Christian Democratic Union (CDU).

Siasa za Ujerumani: Uchaguzi wa mapema wanukia

Kansela Scholz anatarajiwa kuitisha kura ya imani katika bunge la Ujerumani, Bundestag mnamo Desemba 16 ili kuwezesha uchaguzi kufanyika.

Kusambaratika kwa muungano tawala wa vyama vitatu kulichangiwa na hatua ya Scholz ya kumfuta kazi waziri wake wa fedha Christian Lindner.