Uchaguzi wa rais Georgia:
26 Novemba 2003Matangazo
TIBILISI: Nchini Georgia maafisa rasmi wa chama cha upinzani cha Mikhail Saakashvilii wanatarajiwa kumteua kama mgombea wao wa urais. Bunge la Georgia liliteua Jumaane, Januari 4, kama ni siku ya uchaguzi wa rais kufuatia kujiuzulu Eduard Shevardnadze mwishoni wa juma lililopita. Wakati huo huo kaimu rais Nino Burjanadze ameondoa hali ya hatari, na mahkama kuu ya Georgia imefuta matokeo ya uchaguzi wa bunge ambao ulifanyika Novemba Mbili, na ni sababu ya kuzuka misukosuko nchini. Wizara ya kigeni ya Marekani ilisema ujumbe wake utazuru Georgia juma lijalo kuchunguza hali ya mambo katika nchi hiyo.
