Uchaguzi wa rais Lebanon waahirishwa
17 Desemba 2007Matangazo
Uchaguzi wa rais nchini Lebanon umeahirishwa tena kwa mara ya tisa huku nchi hiyo ikikabiliwa na mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa tangu vita vya wenyewe kwla wenyewe kumalizika.
Pande mbili zinazovutana ikiwa ni pamoja na muungano unaotawala na unaoungwa mkono na Marekani na upinzani unaoungwa mkono na Syria, zimekubaliana kuwa kamanda mkuu wa jeshi la Lebanon, jenerali Michel Sleiman, awe rais mpya wa nchi hiyo.
Hata hivyo pande hizo zinalazimika kulisubiri bunge liidhinishe makubaliano hayo. Kura itapigwa Jumamosi ijayo.