1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Uchaguzi wa rais nchini Urusi kumalizika Jumapili

17 Machi 2024

Uchaguzi wa rais nchini Urusi utakamilika hii leo, na Rais Vladimir Putin anatarajiwa bila shaka kujishindia muhula mwingine wa miaka sita madarakani.

Urusi- Uchaguzi wa rais
Bibi raia wa Urusi akipiga kura mjini Moscow katika uchaguzi wa raisPicha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Kulingana na wataalam huru wa sheria za uchaguzi nchini Urusi na hata nje ya nchi, mchakato wa uchaguzi nchini Urusi si wa huru wala haki maana upinzani umetengwa na wagombea watatu walioidhinishwa wanachukuliwa kuwa vibaraka wa Kremlin.

Mjane wa aliyekuwa mkosoaji na mpinzani mkuu nchini Urusi Alexei Navalny, Bi Yulia Navalnaya ametoa wito wa kufanyika maandamano katika ubalozi wa Urusi mjini Berlin ambako Warusi karibu 2, 000 walikusanyika kupiga kura. Uchaguzi huo umefanyika huku vita vikiendelea kati ya Moscow na Kiev.