1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi waanza Zimbabwe

Mwagodi27 Juni 2008

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais imeanza nchini Zimbabe huku taharuki ikitanda kuhusu usalama wa wananchi.

Uchaguzi wa duru ya pili waanza Zimbabwe.Picha: AP

Rais Robert Mugabe wa chama tawala cha ZANU PF ndiye mgombea pekee katika uchaguzi, baada ya aliyekuwa mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha MDC Morgan Tsvangirai kujitoa.

Jumuiya ya kimataifa imesema kuwa haitoitautambua uchaguzi, huo kutokana na ukiukaji mkubwa wa demokrasia unaofanywa na utawala wa Mugabe kuelekea uchaguzi huo.

Tofauti na awamu ya kwanza ya uchaguzi mwezi Machi,ambapo wazimbabwe wengi walijitokeza kupiga kura,leo hii, ni watu wachache tuu walioonekana katika vituo elfu nane vya kupiga kura nchini humo.

Baadhi ya watu waliamua kukaa katika nyumba zao. lakini inaripotiwa kwamba wafausi wa Zanu-Pf wameanza kuwalazimisha wananchi kwenda kupiga kura. Inasemekana bado picha ya mgombeaji wa upinzani Morag Tsvangirai ipo katika sanduku la kura.

Tsvangirai aliyejionda katika duru hiyo ya pili, aliwataka wafuasi wake kutokwenda kupiga kura hiyo aliyoiita ya aibu.

Pia Morgan Tsvangirai ambaye amekimbilia katika ubalozi wa Uholanzi toka Jumapili iliyopita kuhofia maisha yake, ameungana na balozi wa Marekani nchini Zimbabwe,James Mcgee kudai kuwa Rais Mugabe ameweka wanajeshi kuwatia hofu watu wajitokeze wapige kura.

Uchaguzi huo umeshtumiwa na jumuiya ya kimataifa ,lakini rais Mugabe alisema hakuna sauti yeyote ya kimataifa itakayobadili nia yake kuendelea na duru hiyo ya pili ya uchaguzi.

Tayari mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa kundi la nchi zilzoendelea kiviwanda duniani,G-8 wamesema hawatautambua uchaguzi huo.

Mawaziri hao waliokuwa katika mkutano wa siku mbili huko Tokyo waliutaja uchaguzi huo kuwa wa aibu kubwa kwa demokraisa ya Afrika.

Nayo Ufaransa ambayo itakuwa mwenyekiti wa umoja wa ulaya miezi sita ijayo, imeanza harakati za kuwaondoa maafisa wa kibalozi nchini humo.

Tsvangirai,alijiondoa dakika ya mwisho huku akidai,dhidi ya madai ya wafausai wa MDC kutuhumiwa,amabapo watu 90 wameuwawa tanagu uchaguzi wa machi 29. Baadhi ya watu nchini humo wamesema wanahofia maisha yao baada ya ripoti kwamba mmaafisa wa polisi watakaguwa vidole vyao kuhakikisha walipiga kura.

Uchaguzi huu,huenda utampa Mugabe awamu nyengine ya uongozi, lakini pia utaligawanya zaidi taifa hilo amabalo tayari limepewa mbinyo na juuiya ya kimataifa. Marekani,Ulaya,na mataifa ya Afrika yamesema hayatambua uchaguzi huo.



Isabella Mwagodi.