1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchina kuzingatia mustakabali wa Hong Kong.

7 Machi 2004
BEIJING: Kiongozi wa Uchina Hu Jintao ametoa mwito wa kuzingatia mustakabali wa kisiasa wa utawala wake maalumu wa Hong Kong. Lazima udurusiwe tena ule msingi wa kisiasa unaosema kuna nchi moja yeye mifumo miwili ya kisiasa, alisema Bwana Hu Jintao wakati alipokutana na kiongozi wa serikali ya Honk Kong Chee Hwa mjini Beijing. - Hadi sasa Hong Kong imeendelea kuwa na utawala wake wenyewe, isipokuwa sekta za siasa ya mambo ya nje ulinzi zinaendelea kudhibitiwa na Uchina.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW