1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Uchochezi wa vita, ukabila vyatawala kwenye kampeni Kongo

Mitima Delachance12 Desemba 2023

Wakati joto la uchaguzi likizidi kupanda nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, bado ushindani mkubwa unaendelea baina ya wagombea wanaotuhumiana kuchochea vita mashariki mwa taifa hilo pamoja na ukabila.

DRC | Wahlveranstaltung des Kandidaten und amtierenden Präsidenten Felix Tshisekedi
Picha: ARSENE MPIANA/AFP/Getty Images

Kwa kutumia muziki, picha, mabango, ujumbe kwenye redio na runinga au hata pia kwenye simu za mkononi, Wagombea Urais, wagombea ubunge wa kitaifa na majimbo na hata wagombea udiwani wa manispaa wanafanya kampeni zao kujaribu kuwashawishi mamilioni ya watu wa Jongo kupiga kura na kuwachagua ifikapo Desemba 20 siku iliyopangwa kufanyika uchaguzi.

Placide Ntole ni mgombea ubunge wa kitaifa mjini Bukavu, ambae imani yake kubwa ameielekeza kwa vijana katika uchaguzi huo unaofanyika huku upande wa mashariki hali ya usalama ikiwa tete amesema anaimani taifa hilo litachagua viongozi ambao ni wazalendo.

Tangu kuanza kampeni yake, Rais Felix Tshisekedi anayemaliza muhula wa kwanza amewanyooshea kidole baadhi ya wagombea wenzake bila kuwataja majina akiwashutumu kwa kutumiwa na Nchi za kigeni, na wengine kwamba wanaunga Mkono machafuko ya kivita mashariki mwa Congo.

Soma pia:Rais Tshisekedi ana nadi sera zake Tanganyika

Mgombea ubunge wa kitaifa mjini Bukavu, Profesa Pascal Isumbisho ni mwanachama wa Chama cha LGD chake Waziri Mkuu wazamani Augustin Matata Ponyo, anasema wagombea kurushiana vijembe katika majukwaa ya kisiasabadala ya kueleza sera zitazowavutia wakongomani kuwachagua ni kujiua kisiasa.

"Kama yeye si mzalendo anajua wale ambao wanawafukuza maadui ambao hao ndio tunawapenda sisi wakongomani"

Aliongeza kwamba Wakongo kwa sasa wanahitaji utulivu hivyo mwanasiasa ambae sera zake zitaelekea katika kuleta utulivu wa nchi ndio zitavuna kura.

Upinzani watuhumu utawala kufanya hila katika kampeni 

Baadhi ya wagombea wakiwemo Denis Mukwege na Martin Fayulu wameutuhumu utawala waTshisekedi kwa kuwazuia kufanya kampeni zao kama kawaida wakisema wanakabiliwa na tatizo la usafiri wa ndege katika majimbo ya nchini humo.

Wanasiasa hao wameendelea kushusha lawama kwa chama tawala kuwa kuwa kimenunu hazina yote ya mafuta ya ndege ili kutatiza usafiri wa ndege zitakazowabeba wagombea wa upinzani.

Mgombea wa Uruis kutoka upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Martin Fayulu akiwa katika mkutano wake wa siasaPicha: Benjamin Kasembe/DW

Licha ya masikitiko ya upinzani wa kisiasa, vyama vinavyounga Mkono utawala vinasisitiza nia ya Rais Felix Tshisekedi ya kutetea maslahi na uzalendo nchini Congo.

Soma pia:Katumbi: Tshisekedi ameshindwa kuleta amani na utulivu Kongo

Edouard Makala ni mwanasheria ambaye pia ni mwanachama wa chama tawala cha UDPS mjini Bukavu, anahisi kwamba ushindani huu ndani ya kampeni hii hautaathiri kwa lolote mshikamano wa kitaifa baadae:

Wakati huu ambapo baadhi ya wachambuzi wanatilia shaka uwezekano wakufanyika uchaguzi Desemba 20 kwa sababu za kiufundi, Tume Huru ya Uchaguzi CENI imetangaza kwamba imepokea mjini Kinshasa vifaa vya mwisho kutoka China vya kupigia kura.

Shirika la habari la Kongo ACP limetangaza kwamba Ndege na helikopta za Nchi jirani ya Angola zitatumwa nchini humo kusambaza karatasi za kupigia kura na kadi zinazohakikisha matokeo ya kura katika majimbo.

Vyama vya siasa vya upinzani Afrika vimetekeleza wajibu wao?

02:19

This browser does not support the video element.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW