Uchumi wa dunia uko katika "tishio kubwa": Mkuu wa IEA
23 Machi 2026
Akizungumza katika hafla ya Waandishi wa Habari katika mji mkuu wa Australia, Birol aliulinganisha mgogoro wa sasa wa nishati na ule wa miaka ya 1970 na athari za uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine mwaka wa 2022. Mkuu huyo wa IEA amesema kiasi ya vituo arobaini vya nishati vimeharibiwa kwa kiasi kikubwa katika Mashariki ya Kati kutokana na vita katika eneo hilo.
Amesema mambo yalivyo sasa ni kuwa kuna migogoro miwili ya mafuta na mmoja wa gesi, ambayo imeunganishwa pamoja. Birol amesema anatumai kuwa hali hiyo itatuliwa haraka iwezekanavyo akiongeza kuwa IEA inashauriana na serikali za Asia na Ulaya kuhusu kutolewa kwa mafuta ya akiba kama itahitajika. Mataifa wanachama wa IEA walikubaliana Machi 11 kutoa mapipa milioni 400 ya mafuta kutoka kwenye hifadhi za kimkakati ili kupambana na kupanda kwa bei za mafuta ghafi duniani.