1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Uchumi wa Ujerumani waingia katika mdororo

Daniel Gakuba
25 Mei 2023

Mfumko wa bei umeathiri uchumi wa Ujerumani, ambapo walaji wamepunguza matumizi ya vitu kama chakula na mavazi. Ughali wa bei ya nishati uliosababishwa na vita vya Ukraine ni mojawapo ya sababu zinazotajwa.

Opel Arbeitszeit
Picha: AP

Takwimu rasmi zilizochapishwa Alhamisi zinaonesha uchumi wa Ujerumani ulinywea mwanzoni mwa mwaka huu, wakati mfumko wa bei na viwango vya juu vya riba vimepunguza uwezo wa watu kununua mahitaji muhimu katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya.

Shirika la takwimu la shirikisho la Destatis limesema katika miezi ya kwanza ya mwaka 2023 uchumi wa Ujerumani ulipungua kwa asilimia 0.3 kinyume na ilivyokadiriwa awali kwamba umesalia pale pale, bila kupanda wala kushuka.

Kushuka rasmi kwa uchumi wa Ujerumani kumetangazwa kufuatia kunywea kwake pia katika miezi mitatu ya mwisho wa mwaka jana wa 2022. Haya yamefanyika wakati ambapo Ujerumani inakabiliana na ongezeko la bei za nishati kufuatia vita vya Urusi na Ukraine ambapo athari zake zimeshuhudiwa majumbani na hata kwenye biashara.

Licha ya yanayodhihirika kutokana na takwimu hizi, serikali serikali ya Ujerumani imepuuza hofu ya uchumi kudorora kwa muda mrefu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW