1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchunguzi wa ajali ya ndege ya Yemenia waanzishwa Ufaransa

Saleh Mwanamilongo
9 Mei 2022

Mahakama nchini Ufaransa inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi inayohusu kuanguka kwa ndege ya shirika la ndege la Yemen ya mwaka wa 2009 ajali iliyosababisha vifo vya watu 152.

Jemen Aden Internationaler Flughafen
Picha: Saleh Al-OBEIDI/AFP

Uchunguzi wa mahakama unafanyika wakati wawakilishi wa shirika hilo la ndege wakikosa kujiwasilisha katika mahakama hiyo wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini Yemen.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa kipindi cha wiki nne na iwapo watakutwa na kosa watatozwa faini ya euro 225,000 kwa kusababisha mauaji na majeraha kwa binadamu.

Tarehe 29 ya Mwezi Juni mwaka 2009 ndege hiyo aina ya Yemenia chapa 626 ilikuwa inakaribia jiji kuu la visiwa vya la Comoro, Moroni eneo jirani na taifa la Msumbiji na Madagascar kabla ya kuanguka katika Bahari ya Hindi.

Abiria wote waliokuwa wameabiri ndege hiyo walifariki kwenye ajali hiyo isipokuwa Bahia Bakari, wakati huo akiwa mtoto mwenye umri wa miaka 12.

Kati ya abiria 142 waliokuwa kwenye chombo hicho walikuwa wahudumu 11 wa ndege hiyo na raia 66 wa Ufaransa waliokuwa wahehamishwa katika uwanja wa ndege wa Sanaa wakati huo.

Soma pia →Aliyenusurika katika ajali ya ndege ya Yemenia awasili Ufaransa

Kumbukumbu ya ajili 

Picha: AP

Bakari Bahia katika kitabu chake alichokiandika anaeleza yaliomkumba baada ya ajali hiyo kabla ya kuokolewa siku ifuatayo baada ya kukaa  baharini kwa saa kumi na moja.

Ufaransa ilituhumu mamlaka nchini Comoro kwa kuchelewesha uchunguzi wa kubaini chanzo cha ajali hiyo familia za waathiriwa nazo zikiituhumu Yemen kwa kupanga kuhujumu uchunguzi dhidi ya shirika lake la ndege.

Kesi hiyo inaanza kusikilizwa baada ya miaka 13 ya kusubiri haki japokuwa wachunguzi na wataalam wa mambo ya usafiri wa angani walibaini kuwa ndege hiyo haikuwa na changamoto zozote za kiufundi ila wahudumu wake walikosea wakati ndege hiyo ilipokuwa inatarajia kutua jijini Moroni kabla ya chombo hicho hakijapoteza mwelekeo.

Soma pia →Ajali ya ndege.

Karibia watu 560 wamejumuishwa katika orodha ya wanaolalamika, wengi wao wakitokea mjini Marseille kusini mwa Ufaransa nyumbani kwa watu wengi walioathirika na ajali hiyo ya mwaka wa 2009.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW