1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchunguzi wa ajali ya ndege ya DHL waanza

Josephat Charo
26 Novemba 2024

Polisi wamesema mtu aliyekufa alikuwa mfanyakazi wa ndege araia a Uhispania. Wengine watatu, Mhispania, Mjerumani na raia wa Lithuania, wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali.

Mabaki ya ndege ya mizigo ya kampuni ya DHL baada ya kuanguka karibu na uwanja wa Vilnius
Mabaki ya ndege ya mizigo ya kampuni ya DHL baada ya kuanguka karibu na uwanja wa VilniusPicha: Lukas Balandis via REUTERS

Uchunguzi unaendelea baada ya ndege ya mizigo ya kampuni ya DHL iliyokuwa ikisafiri kutokea Ujerumani kuelekea Lithuania kuanguka jana Jumatatu na kuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu.

Mkuu wa huduma za uokoaji na zima moto wa Lithuania Renatas Po·ela amesema ndege hiyo ambayo ilianza safari yake kutoka mji wa Leipzig mashariki mwa Ujerumani ilianguka kilometa chache kutoka uwanja wa ndege wa Vilnius na kuteleza kwa mita kadhaa.

Mabaki yake yaliligonga jengo la makazi na kusababisha moto. 

Po·ela pia amesema eneo hilo halina idadi kubwa ya watu na wakaazi wote 12 waliokuwa ndani ya jengo hilo lililokuwa likiwaka moto wameokolewa wakiwa salama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW