1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UCHUNGUZI WA AJALI YA NDEGE

29 Desemba 2003
COTONOU: Wataalamu wa Kifaransa leo walikichunguza kisanduku cheusi kinachorekodi habari za safari ya ndege,cha ndege ya Boeing 727 iliyopata ajali siku ya Krismasi katika pwani ya Benin.Imethibitishwa kuwa kutoka jumla ya abiria 151 na watumishi 10 wa ndege hiyo ya shirika la Kilibnani UTA,watu 24 wamenusurika.Ndege hiyo iliotokea Guinea ilitua Benin ikiwa njiani kwenda Beirut.Baadhi kubwa ya abiria walikuwa wageni wa Kilibnani waliokuwa wakienda nyumbani kwa mapumziko ya Krismasi.Elfu kadhaa ya Walibnani huishi katika nchi za Afrika ya Magharibi wakihusika na mambo ya biashara na ni nguzo ya uchumi wa nchi hizo za Kiafrika.Miongoni mwa abiria waliofariki ni wanajeshi wa amani 15 wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh.Wanajeshi hao walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kukamilisha ujumbe wao wa kulinda amani nchini Sierra Leone.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW