Uchunguzi wa kimataifa wabaini Korea Kaskazini iliizamisha meli ya Korea Kusini
20 Mei 2010Wachunguzi wa kimataifa wamesema kuwa kombora hilo liliizamisha meli hiyo ya Korea Kusini iitwayo Cheonan March 26 mwaka huu, na kusema mabaki ya kombora hilo yalidhibitisha kuwa lilitoka Korea Kaskazini.Mbali ya kuawa kwa wanamaji 46, wanamaji wengine 58 waliokolewa kutoka katika meli hiyo.
Rais Lee Myung-bak wa Korea Kusini ameahidi kuchukuliwa kwa hatua kali kutokana na uchokozi huo na ameitisha kikao cha dharura cha kamati ya usalama kesho Ijumaa.
Mjini Washington Rais Barack Obama wa Marekani ameahidi ameahidi kuiisadia Korea Kusini kujilinda kutokana na vitendo vyovyote vingine vya uchokozi.Marekani imeunga mkono taarifa ya wachunguzi hao wa kimataifa.Uingereza na Australia pia zimeungana na Marekani katika kuiunga mkono ripoti ya uchunguzi huo wa kimataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema ripoti ya uchunguzi huo, inasikitisha na kuongeza kuwa ofisi yake itaendelea kufuatilia kwa kakribu hali kuhusiana na ripoti hiyo.
China kwa upande wake ambayo ni mshirika wa Korea Kaskazini, ikizungumzia juu ya ripoti hiyo imesema ni tukio la bahati mbaya.Naibu Waziri wa Nje wa China Cui Tiankai ametaka kuimarishwa kwa utulivu na usalama katika eneo la Rais ya Korea.
Korea Kaskazini yenye imekanusha kuhusika na shambulio hilo na kuonya kuwa iko tayari kwa mapambano iwapo vikwazo vipya vitawekwa dhidi yake kufuatia ripoti hiyo.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters,AFP