1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump na Harris wakabana koo kuelekea White House

9 Septemba 2024

Kwa mujibu wa utafiti wa maoni, mbio za kuingia ikulu ya Marekani zinaenda sambamba kati ya Makamu wa Rais Kamala Harris na rais wa zamani Donald Trump.

Picha ya pamoja | Donald Trump na Kamala Harris
Picha ya pamoja ya Kamala Harris na mpinzani wake Donald Trump. Utafiti unaonyesha wapinzani hao wanakwenda sambamba kabla ya mdahalo Picha: Alex Brandon/AP/picture alliance und Mat Otero/AP/dpa/picture alliance

Utafiti huu unatolewa wakati ambapo washindani hao wanatarajiwa kupambana kwa hoja kwenye mdahalo utakaoonyeshwa kwenye televisheni kwa mara ya kwanza.  

Utafiti wa hivi karibuni unathibitisha kwamba Trump anaendelea kuungwa mkono na takriban nusu ya wapiga kura, licha ya sifa mbaya kama mhalifu aliyehukumiwa, na licha ya dhima yake katika kujaribu kuyabadilisha mateko ya uchaguzi wa mwaka 2020 ambapo Rais Joe Biden alishinda.

Hata hivyo, utafiti unaonesha kwamba Harris, bado hajapiga hatua kubwa mbele. Matokeo ya utafiti wa maoni ya wapigakura uliofanywa kwa ushirikiano wa New York Times na taasisi ya utafiti ya Siena yameonesha kuwa katika nchi nzima Trump yupo mbele kwa asilimia 48 wakati Harris ana asilimia 47. 

Utafiti huo wa maoni umeonesha kuwa Kamala Harris, mwenye umri wa miaka 59, anaongoza katika majimbo ya Wisconsin, Michigan na Pennsylvania, na wagombea wa urais wako sambamba katika majimbo mengine manne ya Nevada, Georgia, North Carolina na Arizona.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW