Udhibiti mkali zaidi wa bajeti wahitajiwa Umoja wa Ulaya
13 Mei 2010Mkuu wa masuala ya uchumi na fedha katika Umoja wa Ulaya,Olli Rehn amesema, kuanzia mwaka 2011,miswada ya bajeti za nchi wanachama, iwasilishwe Brussels kabla ya kuidhinishwa na mabunge yake.
Sera za fedha katika Umoja wa Ulaya, lazima ziratibiwe hapo awali, ili bajeti ya nchi moja isijekuhatarisha uchumi wa wanachama wengine. Hata kanuni za miradi ya kuimarisha na kufufua uchumi,zinapaswa kuwa kali zaidi. Kwa njia hiyo, hali ya madeni ya serikali za kitaifa itaweza kudhibitiwa vizuri zaidi.
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ameunga mkono pendekezo hilo la kutaka udhibiti mkali zaidi wa nakisi za bajeti katika Umoja wa Ulaya. Amesema, haamini kuwa hatua hizo kali zinaopunguza mamlaka ya mabunge ya kitaifa.Mfumo mkali wa kusimamia miradi ya kuleta utulivu na kufufua uchumi ni utaratibu ulio sahihi.
Mwandishi: P.Martin/ZPR