1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA, AFC na CONCACAF zamkosoa Infantino

10 Agosti 2026

UEFA, AFC na CONCACAF, zimemkosoa Rais wa FIFA Gianni Infantino kwa kile yaliyokitaja kuwa ukiukaji wa imani na uaminifu katika usimamizi wa masuala ya kibiashara ya Kombe la Dunia.

Canada Vancouver 2026 | Infantino
Rais wa FIFA, Gianni InfantinoPicha: Darryl Dyck/The Canadian Press/AP Photo/dpa/picture alliance

Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), lile la Amerika Kaskazini, Amerika ya Kati na Karibiani (CONCACAF), pamoja na la Asia (AFC), yanaamini kwamba mpango wa hivi karibuni wa Rais wa FIFA, Gianni Infantino, wa kuuza sehemu ya haki za kibiashara za Kombe la Dunia ulikuwa “ukiukaji mkubwa wa imani na uaminifu” kwa taasisi ambazo chombo cha usimamizi wa soka duniani, FIFA, kinapaswa kuzihudumia.

Katika barua ya wazi kwa familia ya soka duniani iliyotolewa Jumatatu, mashirikisho hayo yalisema mpango wa hivi karibuni wa kuuza sehemu ya haki za kibiashara za Kombe la Dunia umeenda kinyume na wajibu wa FIFA wa kuhudumia wadau wa mchezo huo.

Barua hiyo ilieleza kuwa imani inapovunjwa kupitia udanganyifu na kiongozi kujiweka juu ya wadau waliomkabidhi mamlaka, basi huwa ameacha kutekeleza wajibu wake. Mashirikisho hayo pia yalisisitiza kuwa soka ni mali ya jamii ya kimataifa na si ya mtu mmoja au taasisi yoyote.

Taarifa hiyo imesainiwa na Rais wa UEFA Aleksander Čeferin, Rais wa AFC Salman Bin Ibrahim Al-Khalifa, Rais wa CONCACAF Victor Montagliani, pamoja na makatibu wakuu wa mashirikisho hayo matatu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW