1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uefa Euro 2012: Timu zafanya maandalizi ya mwisho

4 Juni 2012

Uingereza inafanya jaribio la mwisho hii leo kabla ya kuingia dimbani katika fainali za kombe la mataifa ya Ulaya, Euro 2012, wakati kocha wa Ujerumani Joachim Loew asema kikosi chake kinahitaji marekebisho makubwa.

epa03204565 (FILE) The mascots of the UEFA EURO, Slavek (L) and Slavko (R), pose in the Donbass Arena stadium during their presentation in Donetsk, Ukraine, 23 November 2010. The stadium in Donetsk will host three preliminary round games, one quarter final and one semi final of the UEFA EURO 2012. EPA/PHOTOMIG *** Local Caption *** 00000402463512 +++picture alliance / dpa
Alama ya fainali za EURO 2012Picha: picture-alliance/dpa

Uingereza inakwaana na Ubelgiji huku kukiwa na taarifa za majeruhi kadha katika kikosi cha kocha Roy Hodgson. Hali ya wasi wasi tayari imetanda katika kambi ya Uingereza kufuatia hatua zisizokuwa na utaratibu mzuri za maandalizi katika mashindano haya baada ya kupata pigo mara mbili kwa kumpoteza Gareth Barry na Frank Lampard baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norway.

Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza Euro 2012Picha: picture-alliance / Back Page Images

Kuwapoteza wachezaji hao wazoefu wa kati kunakiweka kikosi hicho cha kocha Roy Hogdson kuwa finyu zaidi katika eneo hilo, wakati jukumu la nahodha Steven Gerrard na Scott Parker kupata umuhimu zaidi.

Uingereza inafungua mchezo wa kundi D dhidi ya Ufaransa Juni 11, na Hogdson anaweza kusameheka kwa kuwalinda wachezaji wake hao wa kati hadi pale mambo yatakapokuwa hadharani katika uwanja wa Donbass Arena huko Ukraine.

Ureno imo mbioni katika kukinoa kikosi chake pamoja na kurekebisha mbinu hapa na pale kabla ya kuingia dimbani kuumana na Ujerumani. Baada ya sare za bila kufungana dhidi ya Poland na hivi karibuni kutoka sare na Macedonia, Christiano Ronaldo na kundi lake wanataka kupata goli lao la kwanza tangu kikosi hicho kilipoirarua Bosnia- Herzegovina mabao 6-2 katika mchezo wao wa marudio katika kundi B, wakati Ureno inakwaana na Uturuki mjini Lisbon.

Kocha wa Ureno Paulo Bento amesema .

Kocha wa Ureno Paulo BentoPicha: AP

"Lengo letu la kwanza ni kufikia nusu fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya .Baada ya hapo tutaangalia mchezo baada ya mchezo itakuwaje katika michezo yetu mitatu ya mwanzo. Tunatambua kuwa tumo katika kundi gumu, lakini tunataka tunataka kuingia katika nusu fainali kwanza ya kombe la Ulaya".

Kikosi cha kocha Bert van Marwirjk kitaingia dimbani leo jioni kukwaana na Ireland ya kaskazini mjini Amsterdam, leo siku saba kabla ya kutiana kifuani na Denmark mabingwa wa mwaka 1992 wa kombe hilo la mataifa ya Ulaya.

Lakini kocha wa Ujerumani ambaye hivi sasa anakinoa kikosi chake kisaikolojia na mbinu, amekiri kuwa timu yake inahitaji kufanya kazi ya ziada baada ya kusumbuka kwa muda wa dakika 90 na kupata ushindi mwembamba wa mabao 2-0 dhidi ya Israel ambayo inaonekana kuwa dhaifu, katika mchezo wao siku ya Alhamis.

Kocha wa Ujerumani Joachim LoewPicha: Reuters

"Ulikuwa , naweza kusema , mchezo wa kawaida wa majaribio na mtu anaweza kusema katika baadhi ya nyakati kuwa mambo mengi hayakwenda sahihi. katika kipindi cha pili tuliweza kushirikiana vizuri zaidi na kuonyesha lengo letu.Lakini wakati tunaingia katika wiki ya mwisho, na ushindi huu , unatoa nguvu kwa timu yetu".

Kocha wa Italia Cesare PrandelliPicha: AP

Wakati huo huo Italia inasema kuwa itajitoa katika fainali za kombe la mataifa ya Ulaya iwapo itaombwa kufanya hivyo kwa manufaa ya mchezo wa kandanda, amesema kocha Cesare Prandeli jana Ijumaa baada ya madai ya kashfa ya kupanga matokeo kuchafua jina la kikosi cha Squardra Azzurri timu ya taifa ya Italia.

Mawandishi: Sekione Kitojo,

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW