UEFA-EURO 2012
11 Juni 2012Unapowaangalia wanasoka wa Hispania ,kama mtetezi wa kombe la Ulaya na wakati huo huo mabingwa wa kombe la dunia,usishangae kama watu watawaangalia kama wenye nafasi nzuri ya kusonga mbele,japo kama katika kundi lao kuna vigogo mfano wa mabingwa wa zamani wa dunia-Italy na wa Kroatia ambao pia ni wa kuhofiwa.Wanasoka wa Ireland wao hawahesabiwi kama kitisho.Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Vincente del Bosque ingawa anazipokea sifa wanazopewa,hata hivyo anakiri kwa kusema:"Katika kundi letu tuna timu ambazo pamoja na Italy zinajivunia sifa kubwa na timu mbili zilizoingia kifua mbele.Mwaka jana tu ndio tumecheza na Italy na ni timu hatari kabisa."Nyota akina Andrés Iniesta,Xavi,Sergio Ramos na iker Cassilas pamoja na wanasoka wengineo wa Real madrid na FC Barcelona watazidi kuwika.Kwakua wao na timu zao wamepigwa kumbo katika nusu fainali ya kombe la Champions League,watataka kulipiza kisasi na kuonyesha katika kombe la Ulaya,hakuna bora kama wao.
Italy:Nyota za zilizokomaa na vijana wenye kipaji.
Italy haihesabiwi tena miongoni mwa timu hatari,lakini miaka sita baada ya kunyakuwa kombe la dunia mwaka 2006,bado timu hiyo ina wachezaji hodari.Hata hivyo lakini wengi kati ya nyota za "Squadra Azzura" zama zao wameziacha nyuma.Mlinzi wa lango Gianluigi Buffon (ana umri wa miaka 324),mchezaji wa kati Andrea Pirlo(miaka 33) na mpachika magoli Antonio di Natale (miaka 34) wameshakurubia umri wa kutundika jozi ukutani na vijana wanasubiri nafasi yao katika majukwaa ya kimataifa.Kawaida wataliana wanacheza mchezo wa kujikinga.Katika mechi za akuania nafasi ya kushiriki katika kombe la ulaya,katika jumla ya michuano kumi wametwikwa mawili tu.Hata hivyo kuna mechi mfano wa aile dhidi ya Ireland ambapo walimaliza sare bila ya kufungana na ile dhidi ya visiwa vya Färoer ambapo walimaliza kwa moja kwa bila.
LInazuka suala vipi timu ya taifa ya Italy itaweza kuvumilia kishindo kinachotokana na kashfa ya hadaa na udanganyifu katika mechi iliyofichuliwa hivi karibuni.Katika pirika pirika za uchunguzi,hata mshambuliaji wa timu ya taifa Leonardo Bonucci wa tim u bingwa ya Juventus Turin aliingizwa.
Ireland:si kitisho
Kusema kweli Prandeli sio kocha peke yake wa kitaliana atakaeketi katika juu ya benchi katika kundi C.Giovanni Trapattoni "mashuhuri kwa jina la "Maestro",akiwa na umri wa miaka 73 hivi sasa na kujikusanyia mataji yasiyokuwa na idadi,anaeongoza mustakbal wa timu ya taifa ya Ireland tangu mwaka 2008.Michuano ya kombe la Ulaya nchini Poland na Ukraine ni pambano la kwanza ambalo Ireland wamefanikiwa kuingia fainali.Tokea hapo hili ni pambano la pili la kombe la Ulaya ambalo waireland wanashiriki baada ya mwaka 1988.Kama ilivyokuwa wakati ule nchini Ujerumani watoto wa Ireland mlinzi wa lango Shay Given (miaka 36),na wenzake akina John O'Shea (29),Damien Duff (33) na Robbie Keane (miaka 31)wanaweza kutolewa duru ya kwanza itakapomalizika.
Croatia:Nafasi nzuri ya kuingia robo fainali
Hii ni mara ya nne kwa watoto wa Kroatia kuteremka katika fainali za kombe la Ulaya.Timu ya taifa ya Croatia ina wachezaji kadhaa ambao bado wanazichezea timu za ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga au waliwahi kuzichezea timu hizo miaka ya nyuma.Kocha wao pia Slaven Bilic aliwahi wakati mmoja kuichezea timu ya Karlsruhe SC.Ni kundi hatari hili,lakini huwezi kutegemea kuwapata washindani ambao ni wapole." aliwahi kusema.Tumebahatika kupata fursa ya kushindana na mabingwa wa dunia Hispania na mabingwa wa zamani wa dunia Italy."Na watoto wanaoongozwa na nahodha Darijo Srna na mchezaji wa kati Luka Modric wana hakuna anaesubutu kusema wamepwaya.
Mwaandishi:Ziemons,Andreas/Hamidou Oummilkheir
Mhariri:Yusuf Saumu