UEFA kubadilisha mfumo wa kuorodhesha timu
5 Septemba 2014Mojawapo ya mapendekezo yanayotolewa ni kuzingatia kuwapanga moja kwa moja washindi wa ligi zinazorodeshwa katika kiwango cha juu na anayeshikilia Kombe la Champions League miongoni mwa kundi la timu zenye viwango vya juu.
Kwa sasa UEFA inaziorodhesha kwa viwango timu kwa kuzingatia matokeo ya kila timu katika kipindi cha miaka mitano kwenye dimba hilo. Hii inaweza kusaidia kuhakikisha kuwa wakati wa kufanya droo ya mechi za makundi ya Champions League, panakuwa na ushindani mkubwa usiotabirika kwa urahisi kama ilivyo sasa.
Lakini bado mshauri wa ukufunzi wa UEFA Alex FERGUSON anahisi kuwa mabadiliko hayo siyo muhimu. Akizungumza baada ya kuandaa mkutano wa siku mbili wa UEFA uliowaleta pamoja makocha wa vilabu vikuu, kocha huyo wa zamani wa Manchester United alisema haijalishi kundi ambalo kila timu inapangwa, muhimu ni kujizatiti na kutaka kujiondoa katika kundi hilo ili kufuzu katika awamu ya mchujo. Maoni hayo yanaungwa mkono na mwenzangu hapa katika meza ya michezo Sekione Kitojo.
Mimi ni mmoja wa wanaotamani sana na wanatarajia kuwa mfumo wa sasa utabadilishwa haraka iwezekanavyo ili kuifanya Champions League kusisimua na kuvutia zaidi siyo tu kwa UEFA kutengeneza mabilioni ya pesa kupitia utazamaji wa mashabiki
Mwandishi:Bruce Amani/AFP/DPA/reueters
Mhariri:Josephat Charo