1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA: Wachezaji nyota kuhamia Saudia isilete hofu Ulaya

19 Juni 2023

Rais wa Shirikisho la Kandanda Barani Ulaya UEFA Aleksander Ceferin amesema wadau katika kandanda la Ulaya hawastahili kuhofia hatua ya wachezaji mahiri kuhamia Saudi Arabia.

Aleksander Ceferin | UEFA Präsident
Picha: Armando Franca/AP/dpa/picture alliance

Ceferin anasema Saudia inafanya makosa kwa kuwa inaekeza kwa wachezaji nyota ambao wanaelekea mwishoni mwa taaluma zao.

Cristiano Ronaldo na Karim Benzema wametia kibindoni mamilioni ya dola na kujiunga na vilabu vya Saudi Arabia mwaka huu na maombo kama hayo yaliwasilishwa kwa Lionel Messi na Luka Modric ila Messi amejiunga na Inter Miami ya Marekani huku Modric akiamua kusalia Real Madrid kwa msimu mmoja zaidi.

Cristiano Ronaldo akiichezea klabu yake ya Saudia Al NassirPicha: FAYEZ NURELDINE/AFP/Getty Images

Wachezaji wengine zaidi wanatarajiwa kujiunga na vilabu vya nchini humo huku Ruben Neves wa klabu ya wolverhampton Wanderers akiripotiwa kukubaliana na Al Hilal pamoja na Ngolo Kante wa Chelsea na wengine wanaowindwa ni Kalidou Koulibaly na Hakim Ziyech.

Chanzo: AP/DPA

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW