UEFA yaishtaki Feyenoord kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi
6 Machi 2015Tukio hilo lilitokea wakati wa pambano la nyumbani dhidi ya Roma ya Italia ambapo Feyenoord ilipoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-1. Mchezo huo wa marudiano uliahirishwa kwa dakika 15 baada ya vitu kadhaa kutubwa uwanjani .
Katika taarifa yake wiki hii UEFA imesema itaamua tarehe 19 mwezi huu kuiwekea vikwazo kilabu hiyo. UEFA pia itamchukulia hatua mchezaji wa Roma Adem Ljajic kwa kuwachochea watazamaji wakati alipokuwa akisherehekea bao lake. Kamati ya nishamu ya Umoja huo wa vyama vya kandanda barani Ulaya, ilipanga kuwa na kikao cha kumjadili mchezaji huyo kutoka Serbia na kilabu yake ya Roma juma hili.
Mashabiki wa Feyenoord walifanya fujo mjini Roma wakati wa pambano la kwanza dhidi ya Roma na kusababisha kilio kwamba baadhi yasanamu za kumbukumbu mjini humo ziliharibiwa.Roma itacheza na Fiorentina katika duru ya timu 16 za mwisho hapo Machi 12.
Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Josephat Charo