1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SanaaBurkina Faso

Ufaransa haitakata mahusiano na Mali, Niger, Burkina Faso

15 Septemba 2023

Waziri wa utamaduni wa Ufaransa Rima Abdul-Malak amesema nchi hiyo haina nia ya kukata uhusiano wa kitamaduni na Burkina Faso, Mali na Niger.

Waziri wa utamaduni wa Ufaransa Rima Abdul-Malak amesema wataendeleza uhusiano wa kiutamaduni na Mali, Niger na Burkina Faso
Waziri wa utamaduni wa Ufaransa Rima Abdul-Malak(kushoto) akielekea kwenye ufunguzi wa shurehe za ufunguzi wa kituo cha "Maison Gainsbourg" mjini Paris, Septemba 14, 2023.Picha: Alain Jocard/AFP

Kauli ya waziri Abdul-Malak ameitoa baada ya wadau katika sekta ya burudani na sanaa nchini Ufaransa kukosoa uamuzi wa kupiga marufuku ushirikiano na wasanii kutoka nchi hizo tatu za Afrika.

Abdul-Malak amekiambia kituo cha redio cha RTL kuwa, Ufaransa iko wazi na inakaribisha wasanii kutoka nchi mbalimbali, na kwamba hakuna mabadiliko yoyote ya sera juu ya hilo.

Matamshi ya waziri huyo wa utamaduni wa Ufaransa yanaonekana kuondoa msuguano na muungano wa wasanii SYNDEAC, ambao ulitaka kukutana na Abdul-Malak baada ya wizara yake kutoa agizo la kusitisha ushirikiano na kukatisha usaidizi wa kifedha kwa taasisi za sanaa kutoka Burkina Faso, Mali na Niger.

Muungano wa SYNDEAC uliitaja marufuku hiyo "kama kitu ambacho hakijawahi kutokea."