1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Ufaransa inapanga kuwaondoa raia wake nchini Niger

1 Agosti 2023

Ufaransa inapanga kuwaondoa raia wake nchini Niger kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini humo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Ludovic Marin/REUTERS

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa maandalizi ya shughuli hiyo ya kuwaondoa kati ya raia 500 hadi 600 wa Ufaransa walioko nchini humo yanaendelea. Kulifanyika maandamano ya kuunga mkono mapinduzi hayo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo waandamanaji walikusanyika mbele ya ubalozi wa Ufaransa huku baadhi wakiripotiwa kuweka bendera za Niger na Urusi katika ubalozi huo.

Italia yatangaza kutuma  ndege maalumu Niger kuwaondoa raia wake

Ufaransa ina karibu wanajeshi 2,500 nchini Niger. Vile vile, nchi hiyo ni muhimu kwake kwa sababu ya utajiri wake wa madini ya urani. Italia pia imetangaza kwamba itatuma ndege maalum nchini humo kwa ajili ya kuwaondoa raia wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW