Ufaransa kuimarisha usalama wakati wa Euro
20 Mei 2016Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault ameahidi kuwa Ufaransa itatumia uwezo wake wote kuhakikisha ulinzi wa kutosha wakati wa michezo hiyo "Kila kitu kimefanywa kuimarisha usalama wa raia wa Wafaransa kila mahali. Pia bunge limepitisha mswada wa kurefusha hali ya hatari. Ufaransa inajilinda dhidi ya kitisho cha ugaidi, na hilo linawahusu raia wa Ufaransa na wageni wowote, kwa mfano wanaokuja kushiriki katiks Euro 2016, watalii wote. Ni hatua ya kuwalinda wote kwa jumla.
Bunge la Ufaransa limeidhinisha kurefushwa kwa miezi miwili zaidi hali ya hatari iliyowekwa tangu mashambulizi ya kigaidi ya Novemba mwaka jana.
UEFA inapanga kuwaajiri karibu maafisa wa kibinafsi wa usalama 10,000 wakati wa kinyang'anyiro hicho na kila uwanja kati ya 10 vitakavyoandaa utakuwa na maafisa 900 wa usalama watakaoweka ulinzi kwa kila mchuano.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef