1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Ufaransa kutangaza mpango wa ujenzi wa Mayotte

Saleh Mwanamilongo
31 Desemba 2024

Hatua hiyo imefuatia ziara yake kwenye kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi wiki tatu baada ya Kimbunga Chido kusababisha uharibifu mkubwa.

Waziri Mkuu wa Ufaransa kutangaza mpango wa ujenzi wa kisiwa cha Mayotte baada ya Kimbunga Chido
Waziri Mkuu wa Ufaransa kutangaza mpango wa ujenzi wa kisiwa cha Mayotte baada ya Kimbunga ChidoPicha: Adrienne Surprenant/AP/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Ufaransa François Bayrou anatarajiwa kuzindua mpango kabambe wa uokoaji na ujenzi wa kisiwa cha Mayotte. Hatua hiyo imefuatia ziara yake kwenye kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi wiki tatu baada ya Kimbunga Chido kusababisha uharibifu mkubwa. Bayrou, aliyeteuliwa hivi karibuni kama waziri mkuu, pia alielezea idadi ya vifo kuwa ni watu 39 lakini alihimiza tahadhari, akisema idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Waziri Mkuu huyo wa Ufaransa amesema rasimu ya sheria ya dharura inayolenga kuijenga upya Mayotte ndani ya miaka miwili itawasilishwa bungeni mwezi Januari.

Ziara ya Francois Bayrou inafuatia ile ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, huku baadhi ya wakaazi wa Mayotte wakiidai kuwa serikali ya Ufaransa ilikuwa imewasahau kwa muda mrefu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW