1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa: Maandamano dhidi ya mageuzi ya pensheni

11 Februari 2023

Maelfu ya raia wa Ufaransa wameandamana sehemu mbalimbali za nchi hiyo ili kupinga mpango wa serikali wa marekebisho ya sheria ya pensheni .

Frankreich Paris Protest gegen Rentenreform
Picha: YVES HERMAN/REUTERS

Maandamano yalianzia huko Nancy na kisha mashariki mwa nchi huko Strasbourg na baadae Toulouse ambapo vyama vya wafanyakazi vinadai kuwa zaidi ya waandamanaji 100,000 waliitikia wito huo, na kuonya kuwa viko tayari kuzuia shughuli zote nchini Ufaransa katika wiki zijazo ikiwa maombi yao hayatosikika.

Hii ni mara ya nne katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja ambapo Wafaransa wametakiwa kuandamana dhidi ya mageuzi hayo ya uongozi wa Rais Emmanuel Macron ambaye amesema kuwa mageuzi hayo ni muhimu ili kudumisha uwezo wa mfumo wa pensheni nchini Ufaransa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW