1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa: Muungano siasa za shoto wamkosoa raia Macroo

11 Julai 2024

Muungano wa siasa za mrengo wa kushoto Ufaransa umemkosoa Rais Emmanuel Macron baada ya kutoa wito wa kuundwa kwa serikali ya mseto ya vyama vingi, wakitaka muungano wao pekee ndiyo upendekeze jina la waziri mkuu.

Paris, Ufaransa | Rais Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Hakuna muungano ambao ulitoa mshindi wa moja kwa moja  katika duru ya pili ya uchaguzi wa bunge, ingawa muungano mkubwa wa Wasoshalisti, Wakomunisti, Watetezi wa Mazingira, na chama cha LFI, chenye kufuata siasa kali za mrengo wa kushoto, ndiyo ulipata idadi kubwa ya viti kulivyo vyama vingine. 

Muungano huo ulipata viti 193, katika bunge la taifa lenye viti 577. 

Soma pia:Rais Macron atoa wito kwa vyama vikuu kushirikiana katika kuunda serikali thabiti ya Ufaransa

Katika barua ya wazi kwa wapiga kura, Macron alisema jana kuwa hakuna mtu aliyeshinda uchaguzi. 

Macron amevitolea wito vyama kutafuta muafaka kwa ajili ya kuunda serikali ya mseto.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW