Ufaransa na Italia zaungana na Uingereza kupeleka maafisa Libya
21 Aprili 2011Ufaransa imesema inapeleka kundi la maafisa wataalamu watakaotoa ushauri wa kiufundi, mawasiliano na mipangilio mizuri.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague amesema mjini London kuwa nchi hiyo itapeleka washauri wa kijeshi 12 nchini Libya, lakini hawatahusika na kutoa mafunzo au kuwapatia silaha waasi au kusaidia shughuli za mipangilio yao.
Katika mkutano na waandishi habari, afisa mkuu wa jeshi la NATO, Admiral Russel Harding amesema jana kuwa jumuiya hiyo imewekewa mipaka na Umoja wa Mataifa ya kuwalinda tu raia.
Wakati huo huo, mjini Geneva Kamishna wa tume ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay ameulaani uongozi wa Libya kwa kutumia mabomu mtawanyiko katika mji wanaouzingira wa Misrata.
Bibi Pillay, amesema kwamba mashambulio kama hayo kwenye maeneo yenye watu wengi yanaweza kuwa uhalifu wa kimataifa.