1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yakaribisha mazungumzo kati ya Xi na Zelenskiy

26 Aprili 2023

Marekani na Ufaransa zimeyakaribisha mazungumzo ya kwanza kwa njia ya simu kati ya rais Xi Jinping wa China na Volodomyr Zelensky wa Ukraine.

Bildkombo Selenskyj und Xi Jinping
Picha: Ukrainian Presidentia/IMAGO/MONCLOA PALACE/REUTERS

Hata hivyo Washington imetadharisha kuwa bado ni mapema kufahamu iwapo yatasaidia kuleta amani.

Ufaransa ilikuwa nchi ya kwanza kusifu mazungumzo hayo ikisema inaunga mkono juhudi zote zitakazosaidia kumaliza vita vya Ukraine na ambazo zinazingatia maslahi ya serikali mjini Kyiv na sheria ya kimataifa.

Kwa upande wake msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa nchini Marekani John Kirby amewaambia waandishi habari kuwa mazungumzo kazi ya Xi na Zelensky ni jambo zuri lakini haijabainika kama yatakuwa na mchango wa kumaliza vita.

Mazungumzo hayo ya viongozi hao wawili yameshuhudia Ukraine ikimteua balozi mpya wa China na rais Xi Jinping akiahidi kumtuma mjumbe wa amani kuitembelea Kyiv kufungua njia ya mashaurino ya kuushughulikia mzozo unaoendelea

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW