Ufaransa na Moroko wanajiandaa kwa mechi ya kihistoria
14 Desemba 2022Wafuasi wanapanga mikusanyiko katika mabaa kutoka kwenye barabara kuu za Paris hadi mitaa ya mji mkuu wa Moroko Rabat, kutoka mji wa Nice hadi mji wa kihistoria wa Morocco wa Marrakech.
Morocco ilikuwa chini ya utawala wa Ufaransa kuanzia 1912-56, na mechi kati ya timu hizi mbili inaibua mvuto wa kisiasa na kihisia kwa mataifa yote mawili.
Mashabiki wataweza kukusanyika ili kutazama pambano hilo kwa wingi na luniga kuwekwa katika viwanja vya umma katika miji karibu yote Moroko, wakati wengi pia watakuwa wakiangalia kutokea nyumbani au kwenye mikahawa.
Mamlaka ya jiji la Paris imesema itaweka maafisa wa polisi 2,000, polisi 800 zaidi waliwekwa Jumamosi usiku kwa robo fainali, wakati Ufaransa walipowashinda wapinzani wao wa kihistoria England mabao 2-1.
Matokeo yatakuaje?
Baadhi ya viongozi wa Ufaransa walitoa wito wa kufungwa kwa mtaa wa Champs-Elysees , ingawa hilo hatimaye lilikataliwa na serikali ya Jiji la Paris.
Vyovyote vile matokeo yatakavyokuwa, sherehe kubwa zinatarajiwa nchini Moroko, kuangazia jinsi walivyoweka historia katika uwakilishaji kwenye michuano ya kombe la dunia.
Morocco imevuka matarajio yote nchini Qatar kwa kuipiga Ubelgiji iliyoshika nafasi ya pili katika hatua ya makundi na kisha kuiondoa Uhispania na Ureno katika awamu ya mtoano na robo fainali kufika nusu fainali.
Mafanikio ya timu hiyo yanaashiria mara ya kwanza kwa nchi ya Kiarabu na Nchi ya Afrika imefuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Kwa wengi mechi dhidi ya bingwa mtetezi ni fursa ya kuonyesha kwamba Moroko ni adui mkubwa kwenye uwanja wa soka angalau, ingawa uhamiaji kati ya nchi hizo mbili umefifisha mipaka kwa wengi nchini Ufaransa na Moroko kuhusu nani wa kumuunga mkono katika fainali hiyo.