1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUfaransa

Ufaransa na Ujerumani kusherehekea miaka 60 ya uhusiano wake

18 Januari 2023

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine pamoja na kubadilika kwa mifumo ya uendeshaji wa siasa za kilimwengu ni mambo yanayoudhoofisha uhusiano kati ya Ujerumani na Ufaransa.

Frankreich | Emmanuel Macron und Olaf Scholz
Picha: Sarah Meyssonnier /REUTERS

Tuanze kwa kuitazama historia ya nchi hizi mbili kubwa barani Ulaya, mwaka 1963 Januari 22 Ufaransa na Ujerumani zilisaini rasimu ya maridhiano baada ya kumalizika vita vya pili vya dunia kupitia waliokuwa viongozi wa nchi hizo wakati huo Konrad Adenauer na Charle de Gaulle,na makubaliano hayo yalijumuisha ushirikiano wa kijeshi,na kuleta uthabiti katika Umoja wa Ulaya.

Januari 22 Kansela wa Ujerumani wa hivi sasa Olaf Scholz anatarajiwa kwenda Paris kukutana na mwenzake Emmanuel Macron kabla ya wote kuongoza mkutano wa pamoja wa mabaraza yao ya mawaziri,kuadhimisha mkataba wa Elysee uliosainiwa mwaka 1963.

Japokuwa mahusiano baina ya viongozi hao wawili yanaonekana kuwa mazuri zaidi ipo mitizamo tafauti inayotolewa pande zote mbili. Mwanachama mmoja wa ngazi za juu katika chama cha Renaissance cha  rais Macron ambaye ameomba jina lake libanwe amewaambia waandishi habari wiki hii kwamba Kansela Scholz  sio mtu anayeupenda kabisa Umoja wa Ulaya,zaidi anaitazama kwanza nchi yake Ujerumani.

Kansela wa Ujerumano Olaf Scholz na Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Mtafiti mmoja katika baraza linalohusika na masuala ya kigeni la Ujerumani DGAP,mjini Berlin,Jacob Ross, anasema nchini Ufaransa kuna hisia zinaonekana kuiangalia  Ujerumani kama nchi isiyoona umuhimu wa mahusiano baina ya Ufaransa na Ujerumani.Misuguano inaonekana  hata na  wananchi wenyewe baada ya  asilimia 36 ya Wafaransa na asilimia 39 ya wajerumani kuhojiwa  na taasisi ya kukusanya maoni ya Ipsos wiki hii na kusema mahusiano ya nchi hizo mbili yako kwenye hali ngumu.

Hata hivyo bado mpaka sasa urithi ulioachwa na mkataba wa mwaka 1963 uliosaniwa mjini Paris baada ya vita vya pili vya dunia unaheshimiwa katika kila nyanja tangu ushirikiano wa kijeshi mpaka utamaduni wa kubadilishana mafunzo kwa vijana wa nchi hizo mbili.

Na sehemu kubwa ya wananchi wa pande zote mbili wanaamini ushirikiano kati ya Ufaransa na Ujerumani ni muhimu kwa Umoja wa Ulaya.Muhula wa kwanza wa rais Macron kuanzia mwaka 2017 uligubikwa na mitizamo ya kukoselewa wakati kiongozi huyo mwenye kufuata siasa za mrengo wa kati alipokuwa akijaribu kurudisha imani ya kiuchumi mbele ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya mjini Brussels wakati mwingine kupitia mageuzi mageuzi ambayo hayakuungwa mkono.

Na hatimae mahusiano yake mazuri na mtangulizi wa Kansela Scholz,Angela Merkel ulimsadia kupata uungwaji mkono  ndani ya Umoja wa Ulaya katika janga la virusi vya Corona.Kiongozi huyo wa Ufaransa pia amefanikiwa kuwavuta upande wake washirika  wengine katika Umoja wa Ulaya,akisaini mikataba ya ushirikiano na Italia na Ugiriki mnamo mwaka 2021 na wiki hii amesaini na Uhispania.Kwahivyo Ross anasema ikiwa itakuwa vigumu hivi sasa kushirikiaana na Ujerumani na kushindwa kusogea mbele,kama anavyotarajia huenda rais huyo wa Ufaransa akajaribu kutafuta washirika wengine mbadala.

Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Albert Cara/AA/picture alliance

Tafauti zilizopo kati Ufaransa na Ujerumani zimejitokeza waziwazi tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo mwezi Februari mwaka jana ambapo mwanzoni nchi zote mbili zilijiepusha kuikosoa sana Urusi ,ambayo ni msambazaji mkubwa wa gesi asilia wa Ujerumani na ambayo Ufaransa ikiitazama  kama mdau muhimu katika siasa za dunia.

Soma pia: Mkataba wa Urafiki kati ya Ujerumani na Ufaransa

Lakini kadri vita vinaongezeka,Ufaransa ikatuma silaha nzito nzito nchini Ukraine kabla ya Ujerumani mnamo mwezi Aprili mwaka jana na mwezi huu ikatangaza inapeleka vifaru vya kijeshi kabla hata ya Marekani na Ujerumani kuamua kupeleka magari ya kivita .

Na hatua hiyo ilionekana kutowapendeza wanasiasa mjini Berlin,kiongozi wa chama cha Scocial Demokratic SPD cha Kansela Scholz, Lars Klingelbell akatoa malalamiko akisema ingetowa ujumbe mzito ikiwa nchi zote tatu zingetangaza uamuzi wao wakati mmoja pamoja.Kama zilivyo Uingereza na Poland,Ufaransa nayo pia inaishinikiza Ujerumani kupeleka silaha-Ukraine vifaru vya kivita chapa Leopard nambari 2 huko Kiev.

Kwa kiasi kikubwa hivi sasa nchi hizi mbili zinatafautiana na baadhi ya wadadisi wanatahadharisha kwamba katika kipindi cha miaka 10,15 au 20 ijayo ni watu wachache watakaokuwa kwenye nafasi ya kujenga maelewano ya dhati  baina ya washirika hao wawili.