1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Ufaransa, Ujerumani, Uingereza zalaani Iran kuhusu nyuklia

15 Juni 2024

Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimelaani kile zilichokiita hatua za karibuni zaidi za Iran, baada ya shirika la atomiki la Umoja wa Mataifa, IAEA, kusema nchi hiyo imetanua uwezo wake wa kinyuklia.

Urutubishaji wa madini ya urani nchini Iran
IAEA ilisema Iran ilikuwa inaimarisha urutubishaji wa madini ya urani katika vituo vyake viwili.Picha: West Asia News Agency/REUTERS

Washirika hao watatu wamesema hatua za Irak zinadhoofisha makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kuhusu mpango wake wa nyuklia. IAEA ilisema siku ya Alhamisi kwamba Iran ilikuwa inaimarisha urutubishaji wa madini ya urani katika vituo vyake viwili.

Ukosoaji huo unajiri zaidi ya wiki mbili baada ya mataifa hayo kuwasilisha azimio katika mkutano wa bodi ya magavana wa IAEA, linalokosoa kukosekana kwa ushirikiano na shirika hilo kutoka kwa Iran, katika hatua ya kwanza kama hiyo tangu Novemba 2022.

Soma pia: Iran yasema mazungumzo na mkuu wa IAEA yalikuwa mazuri

Iran ililikosoa azimio hilo na kulitaja kuwa la kukurupuka na lisilo na busara, na inakanusha madai ya kutengeneza silaza za nyuklia, ikisema mpango wake wa atomiki ni kwa matumizi ya amani na ya kiraia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW