Ufaransa, Ujerumani kuipa msaada wa ulinzi wa anga Ukraine
29 Agosti 2025
Matangazo
Katika taarifa ya pamoja nchi hizo zimesema licha ya juhudi kubwa za kidiplomasia, Urusi haijaonesha nia ya kuvimaliza vita dhidi ya Ukraine. Ahadi ya nchi hizo mbili kwa umoja wa Ulaya imetolewa wakati wa mutano wao wa pamoja uliowakutanisha Rais Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz huko Touloun Ufaransa. Nchi hizo zimeahidiana pia kuboresha zaidi ushirikiano wao katika masuala ya usalama. Hayo yanajiri wakati mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakiwa mjini Copenhagen kujadili namna ya kuiunga mkono zaidi Ukraine iliyo vitani na Urusi.