1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yaadhimisha miaka 10 ya shambulio la Charlie Hebdo

7 Januari 2025

Ufaransa inaadhimisha leo kumbukumbu ya miaka 10 tangu lilipotokea shambulio baya dhidi ya ofisi za gazeti la kuchapisha dhihaka la Charlie Hebdo.

Ukura wa mbele wa CHARLIE HEBDO miaka 10
Ukurasa wa mbele wa Jarida la Charlie Hebdo, miaka 10 baada ya kushambuliwaPicha: Jean-François Frey/PHOTOPQR/L'ALSACE/MAXPPP/dpa/picture alliance

Tukio hilo lilisababisha mshtuko mkubwa nchini Ufaransa na kupelekea kuzuka mjadala mkali kuhusu uhuru wa kujieleza pamoja na uhuru wa kidini. Gazeti hilo lilichapisha katuni ya kumdhihaki kiongozi wa Kiislamu, mtume Mohammad.

Soma pia: Kesi ya shambulizi la Charlie Hebdo yaanza kusikilizwa

Rais Emmanuel Macron na meya wa mji wa Paris Anne Hidalgo wanajiandaa kuongoza maadhimisho ya kumbukumbu hizo katika eneo zilikokuweko ofisi za gazeti hilo, ambalo lilivamiwa na washambuliaji wawili, waliofungamanishwa na kundi la kigaidi la Alqaeda waliojifunika nyuso zao wakiwa na bunduki aina ya AK-47.

Watu 12 waliouwawa katika tukio hilo baya wakiwemo wahariri wa gazeti hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW