1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yachunguza mauaji

22 Machi 2012

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema uchunguzi umeanzishwa kubaini iwapo Mohammed Merah, mshukiwa wa mfululizo wa mauaji, yanayodaiwa kuchochewa na itikadi kali ya dini ya kiislamu, alikuwa na washirika wowote.

France's President Nicolas Sarkozy is seen making a statement on French national television from the Elysee Palace in Paris, in this still image taken from video, March 22, 2012. Sarkozy commented on the ending of the Toulouse standoff in which the 23-year-old gunman suspected of killing seven people in southwestern France in the name of al Qaeda, jumped from a window to his death in a hail of bullets after police stormed his apartment on Thursday. REUTERS/France Television (FRANCE - Tags: POLITICS)
Rais wa Ufaransa, Nicolas SarkozyPicha: Reuters

Rais Sarkozy pia amesema mtu yeyote nchini humo atakayepatikana akitembelea mara kwa mara mitandao inayounga mkono ugaidi ama kuchochea chuki au machafuko, ataadhibiwa kisheria. Rais huyo wa Ufaransa ameahidi kuanzishwa msako wa yeyote atakayekwenda katika nchi za kigeni kwa azma ya kupata mafunzo ya nadharia ya ugaidi.

Sarkozy alikuwa akizungumza baada ya mshukiwa wa mauaji ya watu 7 katika mji wa kusini wa Toulouse kupigwa risasi na polisi na kuuwawa baada ya mkwamo wa saa 32 wakati polisi hao walipojaribu kumkamata.

Mshukiwa huyo Mohammed Merah mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria, alishutumiwa kuwaua watoto watatu wa shule na mwalimu katika shule ya kiyahudi siku ya Jumatatu, pamoja na mauaji ya wanajeshi watatu wa Kifaransa mapema mwezi huu.

Mwandishi: Amina Aboubakar

Mhariri: Josephat Charo