1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yaomboleza wahanga wa kimbunga huko Mayotte

23 Desemba 2024

Ufaransa imefanya maombolezo ya kitaifa leo Jumatatu kwa ajili ya watu waliopoteza maisha katika visiwa vya Mayotte vilivyokumbwa na kimbunga Chido.

Frankreich Mayotte I nationaler Trauertag für die Opfer des Zyklons Chido, Marcon
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron wakisimama kwa dakika moja ya ukimya Jumatatu, Desemba 23, 2024 katika Ikulu ya Elysee, huko Paris, Ufaransa.Picha: Thomas Padilla/Pool via REUTERS

Mapema leo Rais Emmanuel Macron na mkewe Brigitte walikaa kimya kwa muda kutoa heshima zao wahanga wa huko Mayotte, kisiwa masikini zaidi cha Ufaransa ambapo takriban watu 35 walipoteza maisha na wengine 2,500 walijeruhiwa kutokana na athari za kimbunga chido. Mamlaka zinasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka. Maombolezohayo yamefanyika katika wakati nchi hiyo inayoshuhudia msukosuko wa kisiasa mwaka huu inasubiri kutangazwa kwa serikali ya nne ndani ya mwaka huu pekee. Waziri mkuu mpya Francois Bayrou aliahirisha zoezi hilo hapo jana na ripoti za leo kutoka ikulu ya Ufaransa ya Elysee zinasema baraza jipya la mawaziri litatangazwa wakati wowote jioni hii. Hapo kabla Waziri Mkuu Bayrou alisema kwamba anatumai baraza la serikali mpya litatangazwa kabla ya sikukuu ya Krismasi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW