1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yafunga viwanja 12 vya ndege, Ikulu ikihofia ugaidi

20 Oktoba 2023

Ufaransa imekabiliwa hii leo na vitisho vya kuwepo mabomu sehemu mbalimbali na kupelekea mamlaka nchini humo kuchukua uamuzi wa kufunga jumla ya viwanja vya ndege 12 pamoja na Ikulu maarufu ya Versailles.

Flughafen Carcassonne, Bombenalarm Frankreich
Uwanja wa ndege wa Carcassonne ni miongoni mwa vilivyofungwa kwa muda kuhofia mashambulizi ya kigaidi.Picha: Boyer Claude/dpa/picture alliance

Hii ni mara ya tano katika kipindi cha siku chache zilizopita. 

Waziri wa sheria wa Ufaransa, Éric Dupond-Moretti, amesema kuwa miongoni mwa wanaotoa taarifa hizo ni vijana wadogo wasiowajibika na kuongeza kuwa ni wazazi watakaolazimika kulipia hasara kubwa ya kifedha inayotokana na vitendo hivyo.

Soma zaidi: Polisi wafanya msako baada ya kitisho cha bomu Ufaransa

Waziri Moretii amesema hilo halikubaliki na kwamba ni kuzusha hali ya hofu isiyohitajika nchini humo.

Vitisho vya mabomu vimeongezeka nchini Ufaransa ambayo imetangaza hivi karibuni kuwa katika kiwango cha juu zaidi cha tahadhari kwa matendo ya kigaidi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW